Saturday , 2nd Jan , 2016

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limesema halitambui kuvunjwa kwa mkataba wa Haruna Niyonzima na klabu ya Yanga.

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limesema halitambui kuvunjwa kwa mkataba wa Haruna Niyonzima na klabu ya Yanga.

Katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa amesema bado hawajapokea barua kutoka Yanga zaidi ya kulisikia jambo hilo kwenye vyombo vya habari.

Mwesigwa amesema Yanga walipaswa kupeleka swala hilo TFF ili kuwe na pande tatu za kutatua mgogoro huo,kuliko walivyofanya maamuzi ya kipee.

Yanga ilivunja mkataba na Niyonzima mwishoni mwa mwezi desemba mwaka uliopita kwa madai kiungo huyo amekiuka vipengele vya mkataba.
Niyonzima alienda kwenye michuano ya Cecafa Chalange Cup nchini Ethiopia mwezi Novemba mwaka uliopita akiwa na timu ya Taifa lake la Rwanda,na alichelewa kuripoti kambini kwenye klabu ya Yanga baada ya kumalizika michuano hiyo,na ndipo klabu yake ikavunja naye mkataba.

Kamati ya nidhamu ya Yanga ilimwita mchezaji huyo kutoa maelezo ya sababu za kuchelewa kuripoti kambini na ikamtaka ajibu kwa barua lakini Mnyarwanda huyo hakufanya hivo.