Sunday , 29th Jan , 2017

Bao la Luis Suarez dakika ya mwisho limeokoa jahazi la Barcelona na kusababisha kutoka sare ya bao moja na Real Betis katika mwendelezo wa ligi kuu nchini Hispania, La Liga

Luis Suarez

 

Real Betis ilitawala mechi na mchango wao Dani Ceballos na Ruben Castro ukazaa matunda wakati Alex Alegria alipoutumbukiza mpira kwenye wavu.

Awali bao na Barcelona lilikataliwa kutokana kutokuwepo kwa teknolojia ya kutambua bao likivuka mstari wa goli kwenye michuano ya La Liga.

Hata hivyo Suarez alitumia fursa ya kipekee baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Lionel Messi dakika ya mwisho na kusawazisha .

Barcelona wako pointi moja nyuma ya Real Madrid ambao wana mechi mbili za kucheza ikiwemo moja inayochezwa usiku wa leo