Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imewatoa kimasomaso watanzania baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (THE FLAMES) katika mchezo wa awali kufuzu michuano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na Hagi Yebarow Wiish aliyesaidiwa na Hamza hagi Abdi na Salah Omar Abubakar wote wa Somalia, Taifa Stars ilikwenda kupumzika ikiwa tayari ina mabao hayo mawili kibindoni.
Mabao yote yamefungwa na washambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Emmanuel Ulimwengu na Mbwana Ally Samata.
Samatta alianza kufunga dakika ya 18 baada ya kumlamba chenga kipa wa Malawi, Simplex Nthala, kufuatia klosi- pasi ya Ulimwengu kutoka upande wa kulia.
Ulimwengu akafunga la pili dakika ya 22 akiuwahi mpira uliotemwa na kipa Nthala kufuatia klosi ya beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali.
Ushindi huo unaokuja siku moja baada ya Mkwasa kusaini mkataba wa mwaka na nusu Taifa Stars- ni wa kwanza tangu aanze kazi Julai baada ya mechi nne, akitoa sare mbili 1-1 na Uganda, 0-0 na Nigeria na kufungwa 2-1 na Libya.





.jpg?itok=5cvL0YaP)