
Msuva ambaye amekuwa msaada mkubwa katika kikosi hicho kwa misimu miwili iliyopita, sasa anasumbuliwa na malaria, hivyo kufikia kesho hatakuwa fiti kuweza kucheza mchezo huo wa hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Aidha, kocha wa Yanga Hans va Pluijm amekiri kuwa Msuva ataukosa mchezo huo kutokana na kuwa mgonjwa na kudai kuwa anao wachezaji wengine wanaoweza kuziba nafasi yake.
Kukosekana kwa Msuva kunaweza kumpa nafasi kubwa kiungo mshambuliaji ambaye ni mgeni kikosini hapo, Juma Mahadh ambaye amesajiliwa akitokea Coastal Union ya Tanga kupangwa katika mchezo huo japokuwa anaweza kukutana na presha kubwa kwa kuwa siyo mzoefu katika michuano ya kimataifa.
Tayari TP Mazembe ipo jijini Dar es Salaam, ambapo mchezo huo unatarajiwa kupigwa kesho Jumanne kuanzia mida ya saa 10:00 Jioni huku Yanga ikiwa imetangaza kuwa mchezo huo utakuwa hauna kiingilio.