Friday , 5th Jun , 2015

Shirikisho la Soka nchini TFF limeagiza mwakilishi wa Klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba Ramadhan Singano kufika katika shirikisho hilo Juni tisa mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo.

TFF imesema, imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya mchezaji huyo na klabu ya Simba ambapo imetaka kila upande kufika na vielelezo vyake.

TFF imesema, Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo, inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa miguu hapa nchini.