Wednesday , 16th Dec , 2015

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye amesema, katika ukuzaji wa michezo inatakiwa kuangalia sheria upya ili kuweza kupata wawekezaji pamoja na kuweza kulinda wawekezaji.

Nape amesema, ili kuwekeza na kukuza michezo ni lazima sheria hizo zitengenezwe na ziruhusu uwekezaji pamoja na kuwalinda wawekezaji ili kuweza kuendeleza uwekezaji na kuweza kukuza michezo zaidi hapa nchini.

Nape amesema, licha ya sheria za uwekezaji lakini nidhamu pia inatakiwa katika usimamizi wa michezo pamoja na wachezaji suala linalochangia kwa wachezaji kupotea haraka kwa vipaji walivyonavyo kutokana na kukosa nidhamu lakini kama kutakuwa na nidhamu katika michezo wasimamizi pamoja na wachezaji wataweza kupata kile wanachokitarajia katika michezo kwa ujumla.