pichani ni moja ya kadi ambazo mashabiki wa timu za Simba na Yanga watazitumia
Naibu waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Mh. Juma Nkamia ndiye aliyezindua kadi hizo ambapo amesema wizara yake imekua ikizishauri klabu za Simba na Yanga kutafuta njia mbadala ya mapato badala ya kutegemea mapato ya milangoni kwakuwa wanamashabiki wengi kote nchini basi ingekua rahisi kutimiza malengo yao
Aidha Mh. Nkamia amesema kadi hizo zitasaidia mambo mengi kwenye klabu hizo ambayo awali yalikuwa yakichukua muda likiwemo suala la kujua idadi ya wanachama na waliolipia kadi zao za uanachama na pia kadi hizo pamoja na kuwasaidia katika masuala ya kifedha pia zitatumika katika mikutano mikuu ya timu hizo
Kwa upande mwingine naibu waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia amevitaka vilabu vya soka hapa nchini hasa Simba na Yanga kuepuka migogoro isiyo na msingi kitu ambacho kitapelekea mchezo wa soka kukosa udhamini na hivyo kuudidimiza mchezo huo.
Mh. Nkamia amesema viongozi wasio waaminifu na wabinafsi ndio chanzo cha timu hizo kutokuwa na maendeleo pamoja na kuwepo katika medani ya soka kwa muda mrefu huku zikisheheni wingi wa mashabiki kote nchini.