Monday , 4th Jul , 2016

Timu ya Taifa ya vijana Serengeti Boys inatarajia kuwasili nchini saa tisa ya usiku wa kuamkia hapo kesho ikitokea nchini Shelisheli katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.

Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys inatarajia kuwasili nchini saa tisa ya usiku wa kuamkia hapo kesho ikitokea nchini Shelisheli katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chicni ya miaka 17.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF Ayubu Nyenzi amesema, mara baada ya kuwasili nchini timu itakuwa na mapumziko ya muda mfupi na baadaye itaelekea nchini Madagascar kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Afrika Kusini ikiwa ni ahadi ya Rais wa TFF Jamali Malinzi.

Kwa upande wake Kocha wa kikosi hicho Bakari Shime amesema, kambi ya nje ya Madagascar itawasaidia wachezaji kwa ajili ya maandalizi mazuri na pia itavunja mwiko wa kufungwa mara kwa mara na timu za Afrika Kusini.

Serengeti Boys imefanikiwa kusonga mbele katika kuwania ushiriki wa fainali hizo mara baada ya kuichapa kwa jumla ya mabao 9-0 timu ya Taifa ya Shelisheli ambapo katika mchezo wa awali uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 25 mwaka huu Serengeti iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na katika mchezo wa marudiano uliopigwa Shelisheli Julai 02 Serengeti iliibuka na ushindi wa mabao 6-0.