Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India mabao ya Serengeti yalifungwa na Assad Juma katika dakika ya 12 na Maulid Lembe katika dakika ya 87 ambaye alisawazisha baada ya Korea kutangulia kwa mabao 2-1.
Matokeo hayo yanaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi tano na kwamba inasubiri matokeo ya mwisho kati ya Korea Kusini na Marekani yatakayotoa mwanga wa timu itakayocheza nayo.
Mbali ya mchezo wa leo, kikosi cha Serengeti Boys kitashuka dimbani tena Mei 19, 2016 na pia watamaliza dhidi ya Malaysia Mei 21, 2016.
Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25, 2016 na kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India.
India kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.