Monday , 13th Jun , 2016

Kikosi cha Timu ya Taifa ya vijana cha Tanzania Serengeti Boys kinatarajia kuingia kambini hapo kesho badala ya leo kama ilivyopangwa awali kujiandaa na mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana dhidi ya Shelisheli.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, kikosi cha Serengeti Boys kitaanza mazoezi kesho ambapo kinatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza Juni 25 mwaka huu.

Lucas amesema, mara baada ya mchezo huo kikosi kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Julai 02 mwaka huu.

Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya Umri miaka 17 yanatarajiwa kuchezwa hapo mwakani nchini Madagascar.