Tuesday , 15th Dec , 2015

Mshambulizi matata wa Taifa Stars ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mbwana Samatta ametajwa katika orodha ya wachezaji watatu bora na shirikisho la soka la Afrika CAF wanaocheza soka barani Afrika.

Samatta anawania hiyo na wachezaji wengine wawili Baghdad Boundjah wa Algeria na Etoile du Sahel na Kipa machachari wa TP Mazembe ya DR Congo Robert Kidiaba.

Nyota huyo ameingia kwenye kinyang”anyiro hicho baada ya kuwa mfungaji bora wa klabu bingwa barani Africa nae baghdad akiwa kama mfungaji bora wa michuano ya kombe la shirikisho na Kidiaba akiiwezesha Mazembe kutwaa ubingwa wa africa.
Kwa upande mwingine Siku chache tu baada ya kutawazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na shirika la BBC Yaya Toure, ametajwa miongoni mwa wachezaji watatu bora kuwania tuzo ya mwanakandanda bora mwaka huu na Shirikisho la soka barani Afrika .

Nyota huyo wa Manchester City kwa mara nyengine atakuwa akipigania tuzo hiyo dhidi ya mshambulizi wa Black Stars ya Ghana na Swansea Andre 'Dede' Ayew na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund.
Mshindi atachaguliwa na makocha wa timu za taifa na kutangazwa katika dhifa maalum Januari tarehe 7 mwakani.