Kwa kutambua kiu hiyo ya mashabiki wa soka kupata fursa ya kuongelea mchezo huo pendwa duniani, EAST AFRICA TELEVISION, inakualika wewe mpenda soka kufuatilia na kushiriki kipindi cha 'SHABIKI ON SATURDAY' kitakachokuwa kinaruka Mubashara kila jumamosi saa 5:00 asubuhi hadi saa 6:00.
Ndani ya kipindi hicho kuna mambo mengi ikiwemo mtazamaji kupata fursa ya kupiga stori za timu yako kuanzia mechi iliyopita hadi ijayo bila kusahau nafasi ya wewe kushiriki kwa kuonesha uwezo wako wa kuchezea mpira kupitia Challenge.
SHABIKI ON SATURDAY haitaishia kwenye TV pekee bali itakupa fursa pia wewe mtazamaji kutuma video yako kutufahamisha juu ya mchezaji wako unayemkubali kutoka timu ya mtaani kwako au timu ya mtaani unayoikubali.
Mwanadada mwenye kulijua soka la nje ya uwanja, refarii yeye, kocha yeye na nahodha yeye, muite Salama Jabir atakuwa mtangazaji kinara wa 'SHABIKI ON SATURDAY' na itaanza kuruka Jumamosi ya Machi 3, Saa 5:00 Asubuhi kupitia EATV.

