Friday , 29th Jan , 2016

Timu ya Ruvu Shooting inahitaji point moja pekee katika mchezo wake wa Jumapili dhidi ya Lipuli ili kupanda daraja na kurejea ligi kuu Tanzania bara.

Vita ya kuwania kupanda daraja msimu ujao itaendelea wikiendi hii kwa michezo 12 ya Ligi daraja la kwanza nchini kuchezwa katika viwanja mbalimbali kwa makundi A, B, C, kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu.

Jumamosi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, wenyeji Polisi Dodoma watakua wenyeji wa Africa Lyon, Kiluvya United wakiwakaribisha Mji Mkuu (CDA) katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Polisi Morogoro dhidi ya Kimondo FC uwanja wa Jamhuri, huku Kurugenzi ikiwakaribisha Burkinafaso kwenye uwanja wa Wambi mjini Mafinga.

JKT Mlale watawakaribisha Njombe Mji uwanja wa Majimaji mjini Songea, Panone dhidi ya Mbao FC uwanja wa Ushirikia Moshi, Polisi Mara watakua wenyeji wa Rhino Rangers uwanja wa Karume mjini Musoma, huku JKT Oljoro wakiwaribisha JKT Kanembwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Ligi hiyo ya itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo minne kuchezwa, Friends Rangers watakuwa wenyeji wa Ashanti United uwanja wa Karume, Polisi Dar dhidi ya KMC uwanja wa Mabatini Mlandizi, Lipuli wakicheza dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Wambi Mafinga huku Polisi Tabora wakicheza dhidi ya Geita Gold uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mjini Tabora.