Tuesday , 28th Oct , 2014

Timu ya Taifa ya mchezo wa Roll Ball imeiomba Serikali na watu mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kusaidia timu hiyo inayotarajia kwenda nchini Uganda kwa ajili ya kushiriki michuano ya Afro-Asia inayotarajiwa kufanyika Novemba 27 hadi 30 mwaka huu.

Akizungumza na East Africa Radio, Rais wa Chama cha Rolball, Noel Kihunsi amesema timu inaendelea na mazoezi kwa ajili ya michuano hiyo inayoshirikisha nchi mbalimbali ambao ni wanachama wa mchezo huo kutoka Bara la Afrika na Asia.

Kihunsi amesema michuano hiyo ina nafasi kubwa kwa upande wa timu kutoka hapa nchini kutokana na timu hiyo kuwa na rekodi nzuri katika mashindano mbalimbali hususani yale ya michuano ya Kombe la Dunia ambapo mara kwa mara Tanzania imekuwa ikishiriki na kuweza kufanya vizuri.