Kaimu Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla amesema, mashindano hayo yatashirikisha nchi takribani 11 kutoka Afrika mashariki huku Tanzania ikiwakilishwa na jumla ya vijana 27 wakiwa wavulana 16 wasichana 11 watakaoshiriki mbio za kilomita mbalimbali huku wakiwa na makocha 3, meneja wa timu na daktari.
Zavalla amesema, wamechelewa kuanza kambi kwani mpaka sasa wamebakiwa na wiki mbili peke za maandalizi lakini hiyo yote ni kutokana na maandalizi ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya timu lakini wanaamini timu hiyo itafanya vizuri zaidi ili kuweza kubakisha ushindi nyumbani.
Zavalla amesema, siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano hayo watakuwa na mkutano wa viongozi kutoka nchi mbalimbali ili kuwezxa kutoa maelekezo juu ya mashindano hayo.





