Thursday , 19th Feb , 2015

Ligi ya mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es salaam RBA inaendelea kesho katika juma la sita kwa kuzikutanisha timu ya wasichana ya Tanzania Prisons na Vijana Queens matika mchezo wa kwanza ikifuatiwa na timu ya wanaume ya Tanzania Prisons na Vijana.

Akizungumza na East Africa Radio, Mtendaji Mkuu wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam BD, Mohamed Tajiri amesema, michuano hiyo imekuwa na changamoto nyingi hususani katika ushindani ambao ni mkubwa.

Tajiri amesema,timu zote zimeweza kujidhatiti vya kutosha katika majumuisho ya mazoezi kutokana na kila timu kuhitaji kushika nafasi ya kwanza.

Katika michuano hiyo mpaka sasa, JKT inaongoza ikifuatiwa na Pazzy, Sarviour huku Mgulani ikiongozana na Vijana.