Katibu mkuu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe amesema Phiri alitua jijini Mbeya jana jioni, na leo jioni anatarajia kuanza kazi kwa kushirikiana na watu wengine waliopo kwenye benchi la ufundi kwani Meja Mstaafu Abdul Mingange kwasasa yupo mapumziko kutokana na matatizo ya kifamilia yaliyokuwa yakimkabili.
Kimbe amesema moja ya kazi ambazo Phiri anatakiwa kuzifanya ni kuhakikisha anaibakisha timu kwenye ligi kwani matokeo wanayoyapata si mazuri kwao jambo analoamini kwamba litawezekana kutokana na uwezo mkubwa alionao kocha huyo.
Phiri aliyezaliwa miaka 61 iliyopita jijini Blantyre Malawi ndiye aliyemsajili Mrisho Ngassa katika klabu ya Free State.





