Thursday , 2nd Jul , 2015

Aliyekuwa kiungo wa zamani wa Yanga Omega Seme amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Ndanda FC msimu ujao wa ligi kuu Soka Tanzania Bara.

Katika taarifa yake, Afisa habari wa Ndanda FC, Idrisa Bandari amesema, wameridhika na kiwango cha Seme na hivi sasa ni mchezaji rasmi kati ya wachezaji 11 ambao wamepanga kuwasajili kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Bandari amesema, mbali na Omega, wameongeza mkataba wa mwaka mmoja mmoja kwa wachezaji watano ambao bado wanaumuhimu katika kikosi hicho ambapo ni makipa Wilbert Mweta, Kigi Makasi, Masoud Ally, Kasian Ponela, na Hemedy Khoja.