Monday , 29th Jun , 2015

Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga, Nsa Job amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia African Sports msimu ujao wa Ligi kuu Soka ya Tanzania Bara.

Katika taarifa yake, meneja wa African Sports, Abdul Bosnia amesema, wamemsajili Nsa Job ili kuimarisha kikosi chao na wana imani atawasaidia ikizingatiwa kwamba ni mchezaji mzoefu hivyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine waliopo watafanya vizuri.

Job ambaye amewahi kukipiga Villa Squad, Yanga na Simba kwa muda mrefu alikuwa nje ya dimba baada kuvunjika mguu wakati akiichezea Coastal Union mechi ya ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu.