Kocha wa Timu ya Mwadui FC Jamhuri Kihwelo'Julio'
Julio amesema, ameamua kubaki na idadi hiyo ya wachezaji ili kuweza kutoa nafasi kwa wachezaji wake ambao anaamini wote ni bora kuwa na timu katika safari za mikoa husika katika mechi zao watakazocheza kunako ligi kuu Tanzania Bara.
Julio amesema, alikuwa na jumla ya wachezaji 30 hivyo katika zoezi la usajili alichukua wachezaji 13 katika kikosi chake na kuongeza wengine 10 ambao ni wapya.
Kwa upande mwingine Julio amesema, kuelekea Ligi hiyo hawezi kulalamikia ratiba au waamuzi wa michezo kwani kupoteza kwa mchezo hutokana na mapungufu ya kikosi na hata kwa upande wa waamuzi pia wote ni wazuri ila wapo wanaofanya vizuri zaidi na wengine kufanya makusudi katika kuchezesha mechi za Ligi kuu.
Julio amekamilisha usajili wake kwa kuwaacha wachezaji wakongwe aliokuwa nao wakiwemo Nizar Khalfan, Razak Halfan, Jerry Tegete na Athumani Iddi ‘Chuji’




