Monday , 3rd Apr , 2017

Kocha wa Barcelona Luis Enrique amemwita Neymar “mnyama” baada ya mshambuliaji huyo, kufunga bao lake la 100, katika ushindi wa maba0 4-1 dhidi ya Granada.

Neyma akipachika bao 100 katika mchezo

Mshambuliaji huyo wa  kimataifa wa Brazil, alifikia idadi hiyo mabao, katika michezo 177, akimzidi Lionel Messi, mabao 10, kipindi Muargentina huyo, naye akifiksha idadi kama hiyo ya mabao 100.

Enrique, amesema Neymar, ana uwezo wa hali ya juu, na angependa kumuona akifunga mabao mengine 900, ili afikishe mabao 1000, kwa kuwa bado ataendelea kubaki Barcelona.

"Natumai atafunga mabao mengine 900, hivyo tutaendelea kumuona kwenye klabu ya Barcelona kwa miaka mingi ijayo," Alisema Erique.

Ushindi huo unamaanisha Barcelona, wana tofauti alama mbili na vinara wa ligi ya Hisapnia, Real Madrid, inangawa timu hiyo, ya kocha Zidane ina mchezo mmoja mkononi.