Monday , 13th Apr , 2015

Timu ya Taifa ya Mpira wa Netball inatarajia kuingia kambini Mei 17 mwaka huu kujiandaa na mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Juni mwaka huu Nchini Namibia.

Akizungumza na East Afrika Radio, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Netball Nchini, Anna Kibira amesema, timu hiyo inatarajiwa kuingia ikiwa na wachezaji 36 ambapo watakuwa wakipunguzwa kidogokidogo na kufikia idadI ya wachezaji wanaohitajika katika michuano hiyo ambayo inawasilishwa na Chama cha Mpira wa Netball Barani Afrika.

Kibira amesema, wameshatuma barua kwa washiriki kwani wanatakiwa kuingia kambini mapema kwa ajili ya maandalizi ya mshindano hayo ambayo yataipa sifa nchi.