Tuesday , 5th Jul , 2016

Klabu ya Ndanda FC imepanga kuanza zoezi lake la usajili hii leo kwa wachezaji watakaoitumikia klabu hiyo kwa msimu ujao wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Kocha wa Ndanda Malale Hamsini amesema, kwa kuanza klabu hiyo inatarajia kusaini wachezaji wawili kutoka klabu ya African Sports ya Ligi Daraja la kwanza ambao ni Hassani Gurugumu na Ramadhan Pela.

Malale amesema, anaamini usajili wao utakidhi matarajio yao ya kuhakikisha wanafanya vizuri msimu ujao wa Ligi Kuu tofauti na msimu uliopita ambao hawakufanya vizuri.

Malale amesema, msimu uliopita hawakufanya vizuri na kwa kutambua hilo wanahakikisha wanafanya usajili makini utakaokidhi matarajio ya mashabiki wa Ndanda FC.