Thursday , 16th Apr , 2015

Nchi nane zinatarajia kushiriki michuano ya Mpira wa wavu wa Ufukweni kanda ya tano inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Nassor Shariff amesema amejipanga vizuri kwa ajili ya mashindano hayo ambapo ratiba nzima itakamilika usiku na wapo tayari kukutana na timu yoyote.

Nchi hizo shiriki ambazo ni Kenya, Burundi, Rwanda, Misri, Eritrea, Sudan na Somalia ukiacha wenyeji Tanzania zimeshaanza kuwasili nchini kwa ajili ya michuano hiyo ambayo ni ya kuwania kushiriki michuano ya Afrika inayotarajiwa kufanyika Septemba 4-19 mwaka huu, Congo Brazzaville.