Friday , 3rd Jul , 2015

Mwanariadha Alphonce Felix wa mbio ndefu za kilomita 42, anatarajia kushiriki mashindano ya mwaliko ya kimataifa yanayojulikana kama Gold Coast Marathon ambayo yatafanyika mwishoni mwa wiki hii nchini Australia.

Katika taarifa yake, Kocha wa timu hiyo, Francis John amesema, katika kambi wamebaki wanariadha wa mbio ndefu na tayari Alphonce amefanikiwa kupata mwaliko wa kushiriki mashindano hayo ambayo yanalengo la kutafuta viwanmgo vya kimataifa.

Katika mashindano hayo, Alphonce atakuwa na kibarua cha kutengeneza rekodi bora ili kuwezesha kukidhi viwango vitakavyomuwezesha kufuzu kushiriki mashindano ya Dunia ambayo yatafanyika Agosti mwaka huu nchini China.