Monday , 14th Sep , 2015

Shirikisho la soka nchini TFF limesema muda uliobaki ni mdogo kwa Timu ya Taifa kujiandaa na mchezo wa kwanza dhidi ya Malawi kwa ajili ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kugombea kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Katibu mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema, maandalizi yalianza pale walipopata ratiba kwani mchezo huo ni mgumu kutokana na ratiba ilivyo kwani Tanzania mchezo wake wa kwanza itacheza siku ya Jumatano na mchezo wa marudiano utachezwa siku ya Jumapili.

Mwesigwa amesema, makocha Boniface Mkwasa na Hemed Morocco wanaendelea kuangalia maendeleo ya wachezaji huku wakikutana na kujadiliana juu ya alipofikia juu ya utafutaji wa wachezaji watakaoungana katika kikosi cha Timu ya Taifa.