Wednesday , 6th May , 2015

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ameondoka leo kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio.

Uongozi wa Yanga, awali ulipokea maombi kutoka kwaMsuva lakini ulikataa kumruhusu mpaka msimu huu wa ligi uishe ila sasa imeonekana mambo kubadilika na mchezaji huyo tayari ameshatua katika ardhi ya Mandela.

Msuva amekuwa akionesha kiwango bora katika klabu ya Yanga na sasa ndiye anayeongoza kwa utupiaji magoli kunako ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu.