Pamoja na kumpa mikoba Kocha Jackson Mayanja, Simba imeanza kumsaka kocha mkuu na taarifa zinaeleza mzalendo, Hemed Morocco anaweza kuwa bosi mpya Simba.
Wakati Kerr anaondoka, Mayanja tayari yuko Zanzibar na ameanza kazi lakini habari za ndani zinaeleza Simba imefanya mazungumza na Morocco ingawa jambo hilo linafanywa siri.
“Kweli kuna mazungumzo yamefanyika, lakini kila upande unaonekana kuficha sana na hakuna anayekubali hata kidogo kama mazungumzo hayo yamefanyika,” kilieleza chanzo.
“Tena inaonekana wako katika hatua za mwisho kabisa kwani Morocco pia anaonekana yuko tayari,” kiliongeza chanzo.
Morocco ambaye amewahi kuinoa Coastal Union, timu ya taifa ya Zanzibar na sasa ni kocha msaidizi wa Taifa Stars chini ya Charles Boniface Mkwasa.

