Friday , 29th Jul , 2016

Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amefuzu majaribio ya kuichezea klabu ya Mpumalanga inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini lakini kilichomkwamisha ni maslahi madogo.

Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude.

Uongozi wa klabu hiyo umethibitisha kuwa kiungo huyo alikuwa kwenye majaribio kwa muda wa wiki mbili ikiwa ni mara yake ya pili kwenda kwenye majaribio nchini humo amefuzu majaribio hayo.

Aidha, Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, amesema wao waliridhika kumuachia Mkude lakini mchezaji mwenyewe ndiye aliyekataa kutokana na maslahi madogo ya mshahara na fedha za usajili ambazo alitakiwa kupewa.

“Mpumalanga imeshindwa yenyewe kutoa ofa nzuri itakayomshawishi Mkude, hiyo ni baada ya kutangaza kutoa ofa ndogo ambayo mchezaji mwenyewe hakuridhishwa nayo kabla ya kuomba kurejea nchini" - Rais wa Simba, Evans Aveva

Mchezaji huyo aliona ni vigumu kucheza huko kwa mshahara wa shilingi milioni 3 ikiwa bado atahitajika kulipa kodi, hivyo ameona ni bora akaendelea kulipwa mshahara anaoupata hapa nyumbani.