Thursday , 19th Nov , 2015

Jumla ya mikoa 10 imethibitisha kushiriki katika mashindano ya taifa Cup kwa mpira wa kikapu inayotaraji kuanza kutimua vumbi Novemba 22 hadi 29 mwaka huu mjini Dodoma.

Kamishna wa ufundi wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania TBF Manase Zabroni amesema maandalizi ya mwisho kuelekea mashindano hayo yamekamilika licha ya kusuasua kwa wadhamini.

Katika hatua nyingine Manase amesema licha ya kupambana kutafuta fedha kwa kumtumia afisa masoko wao na wengine lakini bado makampuni na mashirika mbalimbali wamekuwa wagumu kuwasaidia licha ya kutoa ahadi za kuwapa sapoti.

Aidha Manase amewatupia lawama baadhi ya viongozi wa mikoa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuuendeleza mchezao huo hapa nchini huku akiamini wameingia kwenye chama hicho kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa.