
Makamu wa Rais wa BFT Wililo Lukelo amesema wao kama BFT wapo katika harakati pia za kuweka kuelekea kwenye mfumo huo ambao unaendeshwa kwa misingi ya kibiashara ili mabondia waweze kunufaika na fursa mbalimbali na kuweza kujipatia kipato rasmi kupitia kwenye kazi hiyo.
Lukelo amesema, mpaka sasa wamefanikiwa kuwasajili mabondia watatu lakini watawasajili mabondia wengine zaidi wenye viwango ili kuendeleza mfumo huo na kuweza kuwatangaza zaidi mabondia hao ambapo aliwataja waliosajiliwa kuwa ni Suleiman kidunda, Haruna Sanga na Sunday Elias.