Wednesday , 9th Apr , 2014

Klabu ya Simba ya jijini DSM, iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya

Ezekiel Kamwaga - Katibu Mkuu wa Simba SC.

Klabu ya Simba ya jijini DSM, iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya katiba yake kufuatia mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika mapema mwezi uliopita katika viwanja vya bwalo la maafisaa wa polisi la Oysterbay.
Akiongea na muhtasari wa michezo, katibu mkuu wa klabu hiyo, bwana Ezekiel kamwaga amesema kimsingi mchakato huo umeshatoka klabuni na uko kwenye ngazi za juu zaidi.
Bwana Kamwaga amesema, kwa sasa, suala la katiba liko kwa msajili wa vyama na vilabu vya michezo kwa ajili ya kuangalia kama kuna vipengele vinavyokinzana na katiba ya nchi, na pia lipo kwa TFF kwa ajili ya kungalia kama kuna vipengele vinavypingana na katiba ya CAF na FIFA.