Saturday , 21st May , 2016

Kikosi cha Mbeya City Wazee wa Komakumwanya kutoka jijini Mbeya wameapa kuwa leo ni siku ya kufunga pazia la ligi kuu kwa ushindi mnono dhidi ya wanakuchele Ndanda FC kutoka Mtwara na kumaliza ligi hiyo kwa heshima na kuwapa zaswadi wana Mbeya wote.

Kikosi cha wagonga nyundo wa Jiji la Mbeya timu ya soka ya Mbeya City.

Kikosi cha Mbeya City Fc leo jumapili kinashuka kwenye uwanja wake wa nyumbani wa kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa kucheza mchezo wa kufungia msimu wa 2015/16 katika ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wageni Ndanda Fc kutoka mkoani Mtwara.

Muda mfupi uliopita Meneja wa kikosi cha City, Geoffrey Katepa ameidokeza mtandao wa klabu hiyo wa mbeyacityfc.com kuwa nyota wote 18 walitayarishwa kwa ajaili ya kuwakilisha timu yao na wako kwenye hali nzuri na tayari kabisa kusaka ushindi mbele ya timu hiyo kutoka kusini mwa Tanzania.

“Jana Mbeya City walimaliza mazoezi jioni ya muda huu wa sa 12, yalikuwa ni mazoezi mepesi kueleka mchezo huo wa leo kila mmoja yuko vizuri na ana ari kubwa, jambo muhimu kwao ni kushinda mchezo huo ili wamalize ligi kwa heshima, amesema hawana wasiwasi wowote na wako salama kwenye msimamo wa ligi, kumaliza kwa ushindi kutawaweka kwenye mapumziko mazuri kwa matayarisho ya msimu mpya," alisema Katepa.

Kuhusu majeruhi Katepa amesema kuwa City itakosa huduma ya nahodha na mlinzi shupavu wa kushoto Hassan Mwasapili aliye majeruhi kufuatia maaumivu ya nyama za paja yanayomkabili, pia Temi Felix na Deo Julius hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho kupisha majeraha waliyonayo.

Mkuu wa kitengo cha utabibu wa timu hiyo Dk. Joshua Kaseko, ameeleza hii leo kuwa watawakosa wachezaji hao kutokana na majereha waliyonayo hii ina maana kuwa wataonekana uwanjani wakati wa matayarisho ya msimu mpya, mwalimu tayari kashafanya utaratibu wa wale wataochukua nafasi zao hivyo wanauhakika wa kuingia uwanjani na kikosi kilicho bora licha ya kutokuwepo kwa nyota hao.