Friday , 14th Aug , 2015

Mashindano ya kutunisha misuli yanatarajiwa kufanyika Agosti 29 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa kushirikisha wachezaji 26 kutoka jijini Dar es salaam.

Katika taarifa yake, Afisa habari anayesimamia michuano hiyo, Philibert Casmir amesema, lengo la kuandaa mashindano hayo ni kuurudisha mchezo huo sambamba na kuibua vipaji vipya hapa nchini.

Casmir amewataka wadau mbalimbali kujitokeza kwa ajili nya kusaidia mchezo huo kurudi katika ramani ya kimichezo ambapo kwa mwaka huu wameboresha mashindano kuliko miaka iliyopita.