
Katika taarifa yake, Mwenyekiti wa TAVA Agustino Agapa amesema, mashindano hayo yatashirikisha timu 16 kati ya hizo nane ni za wanaume na nane ni za wanawake.
Agapa amesema, timu hizo ni Jeshi Stars, Magereza, Jkt, Twalipo zote kutoka Dar es salaam, Mzinga na Moro Stars zote kutoka Morogoro zikiwa zinajumuisha wanaume wna wanawake.
Agapa amesema, pia wanatarajia kupokea timu nyingine kutoka mikoa ya Mwanza, Tanga, Tabora na Arusha ili kuleta hamasa katika mashindano hayo.