Thomas Mashali
Bondia bingwa wa mkanda wa kimataifa wa UBO mtanzania Thomas Mashali simba asiyefugika Rais wa Ghetto ambaye kwa sasa yuko katika mapumziko akiuguza majeraha aliyoyapata kutokana na ajali ya gari amesema bado anathamini mkataba wake aliosaini kupigana na bondia Kalama Nyilawila May 24 mwaka huu.
Mashali amesema ameamua kutoshiriki mpambano huo kutokana na hali ya afya yake kutoimarika na hivyo akawataka mashabiki wake wamwelewe na wampe muda akipona ajiandae na atakuwa tayari kushiriki mpambano wowote atakaoandaliwa na promota wa pambano hilo.
Aidha Mashali amekanusha kukacha pambano hilo eti kwa kisingizoi cha kumwogopa mpinzani wake