Tuesday , 7th Jul , 2015

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime amewataka watu wasiokuwa na shughuli muhimu ya kufanya mkoani humo kutokwenda katika kipindi cha juma hili ili kuepusha usumbufu utakaojitokeza.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime akiongea na waandishi wa habari hawapo Pichani.

Akizungumza leo mjini Dodoma Misime amesema juma hili kuna ugeni mkubwa wa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM ambao unakadiriwa kuwakusanya watu takribani 10,000 ili kuepusha usumbufu utakaojitokeza kama vile kukosa mahali pa kulala ni vema watu wasitishe shughuli zisizo za muhimu mpaka mkutano huo utakapomalizika.

Kamanda Misime amesema wale wote waenye nia ya kufanya uhalifu katika kipindi hicho mkoani Dodoma hawana nafasi kwa kuwa ulinzi umeshakamilika kiasi cha kutosha.

Aidha amewataka wananchi mkoani humo kushirikiana na jeshi la polisi kutoka taarifa pindi wanapopata taarifa ya mtu kutaka kufanya uhalifu na pia wenye nyumba za kulala wageni waweke ulinzi za wa kutosha ili kulinda biashara zao.

Wakati huo huo kamanda Misime amesema barabara ya kwenda jengo la bunge imefungwa jana ikiwa ni rasharasha ya hali ya ulinzi itakavyoimarishwa katika kipindi chote cha mkutano mkuu wa CCM.