Mashabiki wa England na Urusi wakipigana mitaa ya Old Port Jiji la Marseille, baada ya kulewa.
Tabia ya mashabiki wa timu ya soka ya taifa ya England walioonyesha katika mji wa Marseille ni yakusikitisha amesema katibu wa kamati ya Ulinzi nchini Ufaransa Andy Burnham.
Police mjini Marseille walilazimika kurusha mabomu ya machozi ili kuwasambaratisha mashabiki hao ambao walikuwa wamejazana wakati wakisubiri mchezo wa kwanza wa kundi A kati ya Englandna Urusi utakaopigwa usiku huu majira ya saa nne.
Vurugu hizo za mashabiki hao wakingereza zilipelekea mmoja wa maofisa wa polisi kujeruhiwa kwa chupa zilizokuwa zikirushwa na mashabiki hao.
Katika jumbe kadhaa alizotuma katika mtandao wake wa twita, Afisa huyo Mr Burnham amesema vurugu hizo za mashabiki hao zimesababisha mtikisiko mkubwa na inakuwa ni ya kusikitisha mno kuliko ugaidi uliotokea.
Mashabiki wa England wako mjini Marseille wakiwa wanasubiri mtanange wa timu yao dhidi ya Urusi utakaopigwa jumamosi ya leo usiku saa nne katika dimba la city Stade Velodrome na pia watakuwepo wakati timu hiyo ikicheza na Wales siku ya Alhamisi na baadae dhidi ya Slovakia 20 June mechi ambazo zitachezwa huko katika miji ya Lens na St Etienne.