Sunday , 14th Dec , 2014

Baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu nchini wametupa lawama kwa muamuzi wa kike Jonessia Rukya aliyechezesha mechi ya Jana ya Nani Mtani Jembe Dhidi ya Simba na Yanga.

Akizungumza na EATV mmoja wa mashabiki hao, Majuto Bakari amesema mpira ulionekana kumshinda mwamuzi huyo kwani kulikuwa na mazingira ambayo alitakiwa kutoa penati lakini hakufanya hivyo.

Kwa upande wake shabiki mwingine,Ally Hussein amesema mashabiki wanatakiwa kuwa watulivu mara baada ya kuisha kwa mechi na hakuna haja ya kuleta vurugu katika mechi.