Thursday , 28th May , 2015

Mashindano ya majeshi ya mpira wa kikapu CDF Cup yaliyotarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo jana jijini Dar es salaam yameahirishwa kutokana na muingiliano wa ratiba.

Katika taarifa yake, Kocha wa timu ya wanaume ya JKT, Frank Kusiga amesema, mashindano hayo yameshindwa kufanyika baada ya kuingiliana na ratiba ya michuano ya mpira wa kikapu majiji ya Afrika Mashariki na kati yaliyoanza hapo jana uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kusiga amesema, licha ya kuahirishwa kwa mashindano hayo, timu yake inaendelea na mazoezi ambapo wanatarajia mara baada ya kumalizika kwa michuanbo ya majiji wataanza mashindano hayo ya CDF.