Monday , 1st Jun , 2015

Chama cha mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es salaam DRHA kimesema mafunzo kwa wanafunzo juu ya mchezo huo yatasaidia kuweza kupata timu nzuri zaidi za vijasna watakaosaidia kukuza mchezo huo hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio wakati wa mafunzo kwa wanafunzi washiriki wa mchezo yanayotolewa na wakufunzi kutoka nchini Uholanzi, Katibu mkuu wa DRHA Mnonda Magani amesema, kozi hiyo ya wiki moja itasaidia wanafuzni hao kuelewa mbinu na ufunzi kutokwa kwa wakufunzi hao.

Magani amesema, walimu wa mchezo huo wa pia wanapata mafunzo ya vipo vitu vya ziada katika mchezo huo ambavyo hawajawa na uelewa nao ili kuweza kupata nwalimu wazuri wa mchezo huo.

Magani amesema, baada ya kumaliza programu hiyo, itaundwa timu ambayo itacheza mechi ya kirafiki ili kuweza kuangalia viwango vya wanafunzi hao kutokana na mafunzo waliyoyapata kutoka kwa wakufunzi hao.