Friday , 1st Jul , 2016

Ligi ya Mpira wa Magongo ya Mkoa wa Dar es Salaam inatarajiwa kuendelea hapo kesho kwa timu takribani 19 kutimua vumbi Uwanja wa kituo cha kukuza michezo cha JMK Park kidongo chekundu.

Katibu Mkuu wa Chama cha mpira wa Magongo mkoa wa Dar es Salaam DRHA Mnonda Magani amesema, ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi wiki iliyopita imekuwa na muitikio mkubwa kwa mashabiki mbalimbali kujitokeza.

Kwa upande mwingine Magani amesema, katika ligi mbalimbali zilizopita kulikuwa na tatizo la timu shiriki kuchelewa kufika uwanjani hali iliyokuwa ikipelekea timu kufutiwa pointi lakini kwa msimu huu wamefanikiwa kutatua tatizo hilo kwa kupanga ratiba ambayo imesaidia timu zote kufika kwa muda unaotakiwa.