Mechi nyingine tatu zitapigwa hapo kesho ambapo watakutana vinara wa ligi, Mtibwa Sugar na Stand United katika uwanja wa Manungu Morogoro, Tanzania Prisons kuwa wenyeji wa Coastal Union ya Tanga katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, na JKT Ruvu wataikaribisha Ruvu Shooting katika uwanja wa Azam jijini Dar es salaam.
Mzunguko wa nane wa michuano hii utakamilika Jumapili ya wiki hii kwa kupigwa mechi tatu ambapo Yanga itaikaribisha Azam FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mbeya City wataikaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Polisi Morogoro itakuwa wenyeji wa Mgambo uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Hadi ligi kuu inasimama, Mtibwa Sugar ilikuwa ikiongoza kwa Pointi 15 wakifuatiwa na Azam FC na Yanga SC zilizofungana kwa Pointi 13.
Coastal Union ilimaliza ikiwa na Point 11 ikiwa nafasi ya Nne ikifuatiwa na Kagera Sugar yenye Pointi 10 sawa na JKT Ruvu wakati Simba walimaliza na Point Tisa katika nafasi ya Saba sawa na Polisi Moro, Stand United na Mgambo JKT.