Sunday , 31st Jul , 2016

Madereva wawili wa timu moja ya Mercedes, Lewis Hamilton na Nico Rosberg bado wapo kwenye mchuano mkali wa mbio za magari, baada ya hii leo kuchuana tena, na Hamilton, kuibuka kidedea kwa ushindi wa German GP, lakini mwenzake akishika nafasi ya nne.

Lewis Hamilton amejiongezea pointi 19 kwenye mashindano ya dunia baada ya kutwaa ubingwa wa mbio za magari wa German Grand Prix.

Bingwa huyo wa dunia ametwaa taji hilo likiwa la 6 katika mbio 7 alizoshiriki, na anakwenda mapumziko ya kiangazi na ushindi huo mnono.

Dereva mwenza na Hamilton kwenye timu ya Mercedes, Nico Rosberg aliona ni siku mbaya kwenye ardhi ya nyumbani baada ya kupewa adhabu kwa kumlazimisha Max Verstappen kutoka nje ya barabara.