Riziki amesema, wanatarajia kuondoka hapo kesho kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo yatakayoanza kutimua vumbi Februari 16 mwaka huu Nairobi nchini Kenya kwa kushirikisha nchi mbalimbali za Afrika lakini watawaacha baadhi ya wachezaji wenye vigezo lakini wameshindwa kutokana na hali ya kiuchumi.
Riziki amesema, wanaenda kushiriki lakini viti vya walemavu (Wheel Chair) ambavyo vinatakiwa kutumika katika mashindano hayo ni chakavu na kipya kipo kimoja ambacho hakikidhi kutokana na idadi ya wachezaji ambao wanashiriki mashindano hayo.
Riziki amesema, wanaamini licha ya changamoto walizonazo watajitahidi kuweza kufikia malengo wanayoyatarajia katika mashindano hayo.








