Tuesday , 2nd Aug , 2016

Uzuni imewakumba wanafamilia ya mchezo wa ngumi nchini Uganda kufuatia taarifa ya kifo cha ghafla cha kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya ngumi ya nchi hiyo, Dick Katende kilichotokea mapema leo.

Uzuni imewakumba wanafamilia ya mchezo wa ngumi nchini Uganda kufuatia taarifa ya kifo cha ghafla cha kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya ngumi ya nchi hiyo, Dick Katende kilichotokea mapema leo.

Hassan Khalil, ambaye ni kocha mwenza na marehemu, kwenye klabu ya ngumi ya East Cost Boxing huko Naguru, amesema Katende alifariki baada ya kuanguka bafumi usiku wa jana.

Khalili amesema kabla ya hapo, Katende alikuwa mzima wa afya na walikuwa wakiongea kwenye simu juu ya kuiendeleza klabu yao ngumi ya East Coast.

Katende, aliyewahi kuwa bingwa wa Taifa wa ngumi, uzito wa kati, alizaliwa mwaka 1959 huko Missusera Olama, Naguru, na kujiunga na ngumi kwenye klabu ya ngumi ya KCCB Boxing Club 1971.