Thursday , 8th Sep , 2016

Kocha mkongwe wa hapa nchini aliyewahi kufundisha timu mbalimbali ikiwemo timu ya taifa Mohamed Msomari amefariki leo Septemba nane nyumbani kwake barabara ya stesheni mjini Morogoro

Mohamed Msomari enzi za uhai wake

Msomari amefariki kwa kile kinachoelezwa kuwa alikuwa analalamika kusumbuliwa na maumivu ya kifua.

East Africa Radio imefika nyumba kwa marahemu na kuzungumza na ndugu wa marehemu Boma Kilangi, ambaye amesema kuwa marehemu alikuwa akijisikia vibaya kifuani na baadaye aliingia chumbani kwake kwa ajili ya kujipumzisha.

Hata hivyo BOMA KILANGI amesema kuwa Marehemu ameacha watoto watano, pamoja mke wake walioachana mwaka 1983.

Hata hivyo aliyekuwa kocha wa Majimaji PETER MHINA amemzungumzia marehemu enzi ya uhai wake kuwa alimfamu marehemu wakati huo alikuwa mchezaji wa timu ya Majimaji, pia mmoja wa wachezaji waliofundishwa na Marehemu wakati akiwa Moro United, AMANI SIMBA naye alimzungumzia kocha huyo alipokuwa mwalimu wake kwenye klabu hiyo.

, Marehemu atazikwa kesho majira ya saa saba mchana katika makaburi ya kola.

BOMA KILANGI ndugu wa marehemu
Amani Simba