Friday , 11th Sep , 2015

Kocha wa Timu ya wanaume ya Mpira wa Kikapu ya Savio Datti Makula amesema, yupo njia panda baada ya kushindwa kuchagua kikosi cha wachezaji 12 kitakachoshiriki mashindano ya kanda ya tano inayotarajiwa kuanza Oktoba nne mwaka huu nchini Rwanda.

Datti amesema, anapata shida ya kuchagua wachezaji ambao watacheza michuano ya kanda ya tano kutokana na kila mchezaji kuonesha kiwango cha hali ya juu kipindi chote cha mazoezi.

Kwa upande wa timu ya wanawake ya Don Bosco tayari inawachezaji 12 watakaoshiriki michuano hiyo ambapo hivi sasa inaendelea na mazoezi chini ya kocha Mohamed Mchenga.

Kwa upande wake kocha Mchenga amesema, anaamini kikosi chake kitaleta mapinduzi makubwa dhidi ya nchi zote zitakazoshiriki michuano hiyo nchini Rwanda.