Friday , 13th Nov , 2015

Kocha mkuu wa Kagera Sugar Adolf Richard amesema safu ya ulinzi umechangia timu hiyo kufanya vibaya katika mechi 10 za Ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Richard amesema, safu ya ulinzi inaruhusu mabao rahisi na hawana washambuliaji wa maana hata viungo nao pia sio wapambanaji.

Richard amesema, timu haipo vizuri ina upungufu mwingi na inahitajika kufanyiwa kazi kabla ya kuanza kwa mzunguko wa 11.

Richard alichukua jukumu la kuinoa timu hiyo baada ya Mbwana Makata kubwaga manyanga kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo ambapo Kagera iko nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka ikiwa na pointi tano