Tuesday , 23rd Dec , 2014

Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam, hivi sasa inelenga zaidi katika kuendelea kukuza vipaji vya vijana ili kuendelea kukuza klabu hiyo.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Jonas Tobolowa amesema timu haiwezi kuendelea kama haijajenga uwezo binafsi wa kimaslahi na kuendeleza wachezaji hivyo wanaamini kuendeleza wachezaji ni sehemu moja wapo ya kukuza klabu hiyo.

Tibolowa amesema Tanzania kuna wachezaji wengi ambao bado vipaji vyao havijaonekana hivyo iwapo klabu hiyo itawekeza zaidi kwa vijana hao itasaidia kuepuka usajili wa wachezaji kutoka nje ambao wana vipaji sawa na waliopo hapa Tanzania ambao vipaji vyao vimejificha.

Tibolowa amesema vijana hao wakiendelezwa katika vipaji vyao wana uwezo mkubwa wa kuweza kufanya vizuri zaidi ya wachezaji kutoka nje ya nchi, hivyo anaamini wachezaji hao pia wataweza kusaidia timu kwa kuwa ni wazawa katika nchi yao.

Tibolowa amesema licha ya kukuza vipaji vya vijana hao, pia klabu inatarajia kuwa na vyanzo vitakavyosaidia kuipa timu hiyo maslahi yatakayoweza kuikuza na kuitangaza zaidi ili kuweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.